Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Watafufuliwa watu siku ya Kiyama wakiwa peku, uchi, hawajatahiriwa" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanawake na wanaume wote pamoja, kila mmoja anamtazama mwenzake? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Aisha, jambo litakuwa kubwa mno, kuliko hata mtu kushughulika kumtazama mwenzake".
Explanation
Benefits
Msisitizo wa kuwa mwanadamu hatumbukii katika maasi isipokuwa katika hali ya kughafilika; kwani lau akikumbuka ukubwa wa anayemuasi au adhabu zake basi asingeghafilika kumkumbuka na kumshukuru na kufanya vizuri ibada zake hata sekunde moja, na ndio maana utawaona watu siku ya Kiyama wameshughulishwa na nafsi zao, hawatazamani.
Haya kubwa ya wanawake waliokuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa mfano huyu hapa Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anauliza kwa sababu ya aibu, pale anaposikia kwamba viumbe watakusanywa wakiwa uchi wanaume na wanawake.
Amesema Assanadi: Kila mmoja atashughulishwa na jambo lake na wala hatojua hali ya mwenzake, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha" [Abasa: 37] Hakuna yeyote atakayegeuka kutazama uchi wa mwenzake.
Kutahiriwa: Kwa wanaume: Ni kukata ngozi inayositiri kichwa cha uume, na kwa wanawake: Ni kukata kingozi kilichoko juu mahali pa tundu, kinachofanana na kinyama cha jogoo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

