Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia", Pakasemwa: Waonaje ikiwa niyasemayo yako kwa ndugu yangu? Akasema: "Yakiwa kwake uyasemayo utakuwa umemsengenya, na ikiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".
Explanation
Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.
Benefits
Uzuri wa adabu ya Masahaba wakiwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wajuzi.
Kauli ya muulizwaji kwa lile asilolijua: Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Sheria imelinda jamii, na imehifadhi haki na udugu baina yao.
Kusengenya ni haramu isipokuwa katika baadhi ya hali kwa ajili ya masilahi; Na miongoni mwake: Ni kuzuia dhulma, kiasi kwamba atamtaja aliyedhulumiwa yule aliyemdhulumu kwa yule anayeweza kumchukulia haki yake, akasema: Fulani kanidhulumu, au kanifanyia jambo hili na lile, ikiwemo pia kutaka ushauri katika swala la kuoa au ushirika au ukaribu, na mfamo wake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

