Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Explanation
Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu:
La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri.
La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina.
La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.
Benefits
Kumebainishwa sababu za kusalimika katika Dunia na Akhera.
Himizo la mtu kushughulika na nafsi yake anaposhindwa kumnufaisha mtu mwingine, au akahofia madhara juu ya dini yake na nafsi yake endapo atachanganyikana na watu.
Hapa kuna ishara ya kuipa kipaumbele nyumba, na hasa hasa wakati wa fitina, kwani ni katika nyenzo za kuihifadhi dini.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

