Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Barza Al Aslamia -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?"
Explanation
La kwanza: Maisha yake aliyatumia na kuyamaliza katika nini?
La pili: Elimu yake, je aliitafuta kwa lengo la kupata radhi za Allah? na je aliifanyia kazi? na je aliifikisha kwa wenye kustahiki?
La tatu: Mali yake ni wapi aliichuma, je ni katika halali au haramu? Na aliitoa katika mambo gani, ni katika yale yenye kumridhisha Allah au yenye kumchukiza?.
La nne: Mwili wake na nguvu zake na afya yake na ujana wake, aliutumia na kuumaliza katika mambo gani?
Benefits
Neema za Allah kwa waja ni nyingi, na atamuuliza kila mmoja kuhusu neema aliyoishi nayo, hivyo anatakiwa aiweke kila neema ya Allah katika yale yenye kumridhisha.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

