Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa bin Mas'udi radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam, nakuwa imenyooka na kulingana sawa, nakuwa mimea yake: ni (kusema) Sub-haana llaah -Ametakasika Mwenyezi Mungu, Na Alhamdulillaah -Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, Na Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na Allaahu Akbar -Mwenyezi Mungu Mkubwa".
Explanation
Benefits
Fadhila za umma wa kiislamu; kiasi kwamba Ibrahim amani iwe juu yake aliutumia salam.
Himizo la Nabii Ibrahim amani iwe juu yake kwa umma wa Muhammad rehema na amani ziwe juu yake la kukithirisha kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Attwayibi: Pepo ni uwanda (tambarare), kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa fadhila zake akaweka ndani yake miti na magorofa kulingana na matendo ya watendaji; kila mfanyaji atakuwa na nafasi maalum kwa sababu ya matendo yake, kisha Mwenyezi Mungu alipompa wepesi wa kufanya matendo aliyoumbiwa ili azipate thawabu hizo, akamfanye yeye kuwa ni kama mpandaji wa miti hiyo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

