Wamepata ushindi wenye kujitenga
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akitembea katika njia ya kuelekea Makka, akapita karibu na mlima Jumdan, akasema: “Tembeeni huu ni mlima Jumdan, Wamepata ushindi wenye kujitenga” Wakasema: Ni akina nani hao wenye kujitenga ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika Wanaume, na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika wanawake.”
Explanation
Benefits
Kumtaja Mwenyezi Mungu kunaweza kuwa kwa ulimi tu, au kwa moyo tu, au kwa ulimi na moyo pamoja ambayo ni kiwango cha juu zaidi.
Miongoni mwa dhikiri ni nyiradi za kisheria ambazo zimewekewa mipaka, kama vile dhikiri za asubuhi na jioni, na za baada ya sala za faradhi, na nyinginezo.
Amesema Al-Nawawi: Tambua kuwa fadhila za dhikiri hazikomei katika kumtukuza Mwenyezi Mungu (Tasbiih), na tahalil (Laa ilaaha illa llaah), na kumsifu (Tahmiid), na takbir (Allahu Akbar) na mengineyo, bali kila mwenye kumtii Mwenyezi Mungu basi huyo anamdhukuru Mwenyezi Mungu.
Ameeleza Mwenyezi Mungu kuwa miongoni mwa sababu kubwa za kupewa uimara (Thabati), akasema Mtukufu: "Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa." [Al-Anfaal:45].
Sababu ya kufananisha kati ya wanaomtaja Mwenyezi Mungu na Mlima Jumdan ni upekee wake na kujitenga kwake. Mlima Jumdan umejitenga na milima mingine, hivyo hata wanaomkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu wamejitenga pia, mwenye kujitenga ni yule ambaye moyo wake na ulimi wake viko peke yake kwa kumkumbuka Mola wake Mlezi, hata akiwa miongoni mwa watu, na anapata faraja kwa nyakati anazojitenga, na anapata upweke nyakati anazokuwa na watu wengi. Na inaweza kuwa sababu ya kufananishwa mfano huo ni kuwa dhikiri ndio sababu ya uthabiti katika dini kama vile milima ni sababu ya kuimarika kwa ardhi, au ni kwakuwa anakuwa yeye ndiye wa kwanza kupata amali njema duniani na Akhera, kwa sababu msafiri anayetoka Madina kwenda Makka alikuwa anapofika Jumdan, ni dalili ya kuwa kafika Makka, na mwenye kuufikia anakuwa ndiye wa kwanza, basi hivyo hivyo mwenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu yuko mbele ya wengine kwa kumkumbuka kwake Mwenyezi Mungu kwa wingi, na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

