Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Hakiim Bin Hizaam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimuomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanipa, kisha nikamuomba tena akanipa, kisha akasema kuniambia: "Ewe Hakim, hakika mali hii ni kijani kibichi kitamu, atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, basi atabarikiwa ndani yake, na atakayeichukua kwa kujikweza hatobarikiwa ndani yake, na atakuwa sawa na yule anayekula wala hashibi, na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini", Hakim anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ninamuapa yule aliyekutuma kwa haki, sitompunguzia yeyote mali yake baada yako kamwe mpaka ntakapoondoka duniani, akawa Abubakari akimuita Hakim ili ampe chochote, akawa anakataa kupokea chochote kutoka kwake, kisha Omari alimuita ili ampe, akakataa kupokea, akasema: Enyi Waislamu, hakika mimi ninamletea haki yake ambayo Mwenyezi Mungu kamgawia katika ngawira, anakataa kuichukua. Hakim hakumuomba tena mtu yeyote baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mpaka alipofariki Mwenyezi Mungu amrehe
Explanation
Benefits
Kumebainishwa ukubwa wa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba alikuwa akitoa utoaji wa mtu asiyeogopa umasikini kamwe!
Kutoa nasaha na kupupia katika kuwanufaisha ndugu, wakati wa kutoa msaada; kwa sababu wakati huo nafsi huwa imejiandaa kupokea maneno mazuri.
Kujizuia kuwaomba watu, na kuchukia kufanya hivyo, hasa hasa panapokuwa hakuna haja.
Hapa kuna ubaya wa kupupia mali na kuombaomba sana.
Muombaji atakapolazimisha kuomba, hakuna tatizo kumnyima na kumfelisha, na kumpa nasaha, na kumuamrisha kujizuia kuomba, na kuacha pupa ya kutaka kuchukua.
Hastahiki yeyote kuchukua chochote kutoka katika Hazina ya mali za Waislamu isipokuwa baada ya kupepwa na kiongozi, na ama kabla kuwagawanywa kwa ngawira, hastahiki pia kufanya hivyo.
Inafaa kuomba kukiwa na haja.
Amesema bin Hajari: Ndani ya kisa hiki nikuwa, inatakiwa kwa kiongozi kutombainishia muombaji madhara yaliyoko katika uombaji isipokuwa baada ya kukidhi haja yake ili mawaidha yake yafike mahala pake, ili asifikirie kuwa huenda hiyo ndio sababu ya kumnyima shida yake.
Ubora wa Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na kushikamana kwake na ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake.
Amesema Is-haka bin Rahawaihi: Alifariki Hakim radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ulipofikia wakati wa kufa, na hakika alikuwa amekwisha kuwa tajiri mwenye mali nyingi kuliko Makuraishi wote.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

