Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Katada -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndoto njema hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndoto mbaya hutoka kwa Shetani, atakapoota mmoja wenu ndoto mbaya anayoiogopa basi na ateme kushotoni kwake, na aombe ulinzi kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari zake, kwani ndoto hiyo haitomdhuru".
Explanation
Atakayeota yanayomchukiza basi ateme kushotoni kwake, na aombe kinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake; kwani haitomdhuru, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu amefanya hayo yaliyotajwa kuwa ni sababu ya kusalimika na hayo yenye kuchukiza yanayoambatana na ndoto.
Benefits
Migawanyiko ya ndoto: 1- Ndoto njema, nayo ni ndoto ya kweli na ni bishara kutoka kwa Mwenyezi Mungu anayoiona au ikaonwa na mtu mwingine kwake, 2- Mazungumzo ya nafsi, nayo ni yale ambayo mtu huzungumza na nafsi yake akiwa macho (kisha yanajirudia akiwa usingizini), 3- Huzuni na hofu ya Shetani na vitisho vyake ili tu amhuzunishe mwanadamu.
Jambo la msingi katika mambo yaliyotajwa katika milango ya ndoto ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo, na ajipe bishara njema kwayo, na aihadithie lakini kwa yule anayempenda na si kwa anayemchukia.
Na la msingi katika yale yaliyotajwa katika adabu za ndoto mbaya ni mambo matano: Ajilinde kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme pale tu anashituka kutoka usingizini upande wa kushoto mara tatu, na kamwe asiisimulie kwa yeyote, na akitaka kurudi katika usingizi wake basi abadili ubavu aliokuwa awali; kwani ndoto hiyo haitomdhuru.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

