Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakapoota mmoja wenu ndoto anayoipenda basi ndoto hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo, amshukuru Mwenyezi Mungu kwa ndoto hiyo na aisimulie, na akiota ndoto kinyume na hiyo katika yale anayoyachukia, basi ndoto hiyo inatokana na Shetani, basi aombe kinga kutokana na shari yake, na wala asiisimulie kwa yeyote, kwani haitomdhuru".
Explanation
Benefits
Uhalisia wa haya yaliyotajwa katika mlango wa ndoto njema ni mambo matatu: Amshukuru Mwenyezi Mungu juu ya ndoto hiyo, na ajipe habari njema, na aihadithie, lakini asimueleze ila yule anayempenda nasi anayemchukia.
Na uhalisia wa hayo yaliyotajwa katika adabu za ndoto zenye kuchukiza ni mambo matano: Ajikinge kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shari yake, na kutokana na shari ya Shetani, na ateme kushoto mara tatu pale anaposhituka kutoka usingizini mwake, na wala asiisimulie kamwe kwa yeyote, na anapotaka kurejea katika usingizi wake basi ageukie ubavu mwingine tofauti na ule aliokuwa mwanzo; kwani ndoto hiyo wala haitomdhuru.
Amesema bin Hajari: Hekima na lengo la kukatazwa kumsimulia asiyempenda nikuwa endapo atamsimulia huenda akamfasiria kwa mambo yenye kumchukiza, ima kwa sababu ya chuki au husuda, na huenda ikatokea kwa namna ile ile aliyomfasiria au akajiwahi mwenyewe kwa kuanza kuhuzunika na kukosa furaha, akaamrisha kuacha kumhadithia asiyempenda kwa sababu hiyo.
Kushukuru pale zinapotokea neema, na kujirudiarudia kwa mazuri, hilo ni sababu ya kuyadumisha mazuri hayo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

