Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo?" wakasema: Ndiyo, ewe Mtume wa Allah, akasema: "Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri."
Explanation
Maswahaba wakasema: Ndio tunataka hivyo. Akasema:
Ya kwanza: Kueneza na kukamilisha udhu kwa shida; kama vile baridi, ukosefu wa maji, na maumivu ya mwili, na maji ya moto.
Pili: Kupiga hatua nyingi - ambazo ni kati ya miguu miwili- kwenda misikiti iliyo mbali na nyumbani, na kurudi rudi kila wakati.
Tatu: Kungoja wakati wa Swala, na moyo kuambatana nayo, na kujitayarisha kwa ajili yake, na kukaa msikitini kwa ajili yake kungojea jamaa, anaposwali hungojea mahali pake pa kuswali kwa ajili ya swala nyingine.
Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa mambo haya ndiyo Jihadi ya kweli; Kwa sababu yanaziba njia za Shetani juu ya nafsi, na yanatenza nguvu matamanio, na yanaizuia isiingiwe na wasi wasi, hivyo kundi la Mwenyezi Mungu likashinda majeshi ya Shetani kupitia hayo; na hii ndiyo Jihadi kubwa zaidi, kwakuwa imekuwa kama kikosi cha jeshi upande wa maadui.
Benefits
Uzuri wa uwasilishaji wake Mtume rehema na amani ziwe juu yake wa mada na kuwatia kwake hamu Maswahaba zake, kwani alianza kuwatajia ujira mkubwa kwa njia ya kuuliza swali, na hii ni njia mojawapo ya ufundishaji.
Faida ya kuwasilisha suala kwa maswali na majibu: Ili mazungumzo yakite ndani ya nafsi kwa sababu ya utata wake kisha kuyatolea ufafanuzi.
Amesema An-Nawawi, Mwenyezi Mungu amrehemu: Hiyo ndio Jihadi: Maana yake ni Jihadi iliyohimizwa, na asili ya neno (Ribat) ni kufunga kitu, kana kwamba mtu amejifunga kwa ajili ya ibada hizi, na imesemwa kuwa: Ni Jihadi bora, kama ilivyosemwa: Jihadi ni jihadi ya nafsi, na inawezekana kuwa ni Jihadi nyepesi inayowezekana, yaani: ni aina mojawapo ya Jihadi.
Neno “Ribat” lilirudiwa na kufafanuliwa kwa ufafanuzi (Alif na Lam); Hii ni kwa ajili ya utukufu wa matendo haya.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

