Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu?
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu? Akasema: "Usimpe mali yako" Akasema: Wasemaje kama akipigana nami? Akasema: "Pigana naye" Akasema: Wasemaje kama ataniuwa? Akasema: "Basi utakuwa umekufa shahidi". Akasema: Wasemaje kama nitamuuwa? Akasema: "Huyo ataingia Motoni".
Explanation
Benefits
Hadithi ni ushahidi kuwa, elimu kwanza kabla ya matendo, kwa sababu Swahaba alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yanayompasa kabla ya kufanya.
Inatakiwa kwenda hatua kwa hatua katika kupambana na adui kwa mawaidha au kutaka msaada kabla ya kuanza kupigana naye, na ikiwa yeye ndio ataanza kupigana naye, basi hima yake kubwa iwe ni kumzuia na si kumpiga.
Damu ya muislamu na mali yake na heshima yake ni haramu kudhuriwa.
Amesema Nawawi: Tambua kuwa shahidi amegawanyika sehemu tatu; Sehemu ya kwanza ni yule aliyeuliwa katika vita na makafiri kwa sababu yoyote miongoni mwa sababu za kuuawa, huyu anahukumu ya waliokufa mashahidi katika thawabu za Akhera na katika hukumu za dini, nazo nikuwa haoshwi na wala haswaliwi, na wa pili ni shahidi katika thawabu pasina hukumu za kidunia, naye ni aliyekufa kwa maradhi ya tumbo, na aliyekufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali, na aliyeangukiwa na jengo, na aliyeuliwa kwa kutetea mali yake, na wengineo katika wale ambao hadithi sahihi zimekuja kuwaita kuwa ni mashihidi, huyu anaoshwa na anaswaliwa na Akhera atakuwa na thawabu za waliokufa shahidi, na si lazima awe na thawabu sawa na yule wa kwanza, na wa tatu ni yule aliyechukua ngawira kwa siri, na mfano wake miongoni mwa wale ambao dalili zimekuja kuwaondoa kuitwa mashahidi, endapo watauawa katika vita na makafiri, huyu ana hukumu za mashahidi katika dunia, haoshwi, na wala haswaliwi, na wala hana thawabu zao Akhera.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

