Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
Explanation
Benefits
Kuhadithia kuhusu Umma zilizopita kwa yale ambayo yana kheri na mawaidha ndani yake.
Amesema bin Hajari: Hapa kuna kusimama katika haki za Mwenyezi Mungu na rehema zake na kwa viumbe wake, kiasi ambacho amewaharamishia kujiua, na kwamba nafsi ni milki ya Mwenyezi Mungu.
Uharamu wa kutumia sababu zinazopelekea katika kuia nafsi, na onyo kali katika hilo.
Amesema bin Hajari: Na imeonyesha kuwa alijikata kwa ajili ya kujiua na si kwa kutaka kujitibu, ambayo inaweza kuwa dhana ya kunufaika na kitendo hicho.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

