Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadda, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Amesema Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu.
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ibn Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao-Katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "Na wakasema msiwaache waungu wenu, wala msimuache Wadd, wala Suwa'u wala Yaghuth na Yauq na Nasr" Akasema: "Haya ni majina ya watu wema katika watu wa Nuhu, walipokufa shetani aliwajulisha watu wao kuwa wekeni katika vikao vyao ambavyo walikuwa wakikaa hapo masanamu, na yaiteni kwa majina yao, wakafanya hivyo, na hayakuabudiwa, mpaka walipokufa hao na elimu ikasahaulika yakaabudiwa".
Explanation
Benefits
Tahadhari ya kupiga picha na kutundika picha, hasa hasa picha za waheshimiwa.
Tahadhari kutokana na vitimbi vya shetani na kuileta kwake batili katika sura ya haki.
Tahadhari kutokana na uzushi na mambo ya kuzua hata kama lengo la mfanyaji litakuwa zuri.
Nikuwa kupiga picha ni katika nyenzo zinazopelekea katika shirki, hivyo ni lazima kutahadhari kupiga picha za viumbe vyenye roho.
Kujua thamani ya uwepo wa elimu na madhara ya kukosekana kwake.
Nikuwa sababu ya kukosekana kwa elimu ni kufa wanachuoni.
Kutahadhari na kuiga, nakuwa hilo linaweza kumpelekea mfanyaji wake katika kutoka katika Uislamu.
Kutangulia shirki katika umma zilizotangulia.
Nikuwa majina haya matano yaliyotajwa ni katika viabudiwa vya watu wa Nuhu.
Kubainishwa kubebana na kusaidiana watu wa batili juu ya batili yao.
Kufaa kuwaombea mabaya makafiri kwa njia ya ujumla.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

