Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua, Amesema bin Abbas katika aya hii: Washirika, ni ushirikina, uliofichikana kuliko sauti ya mkanyago wa mdudu chungu katika jiwe kubwa jeusi katika giza nene la usiku.
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Msimfanyie Mwenyezi Mungu washirika na hali nyinyi mnajua, Amesema bin Abbas katika aya hii: Washirika, ni ushirikina, uliofichikana kuliko mkanyago wa mdudu chungu katika jiwe kubwa jeusi katika giza nene la usiku". Nayo ni mtu kusema: Namuapa Mwenyezi Mungu na maisha yangu ewe fulani, naapa kwa maisha yangu, na kusema: laiti kisingekuwa kimbwa hiki wezi wangetuvamia, na lau kama si bata huyu wezi wangetujia, na kauli ya mtu kusema kumwambia mwenzie: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka wewe, na kauli ya mtu: lau kama si Mwenyezi Mungu na fulani, usimuweke ndani yake fulani hii yote ina ushirikina".
Explanation
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

