Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na kundi la Ash’ari ili kumuomba atuchukue, akasema: “Wallahi sitokuwa na chochote cha kukubebeni ” Kisha tukakaa muda kidogo aliopenda Mwenyezi Mungu tukae, tukaletewa ngamia, akaamrisha tupewe wanyama watatu kwa ajili yetu, tulipoondoka wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: Mwenyezi Mungu hatotubariki, tumemuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamuomba atubebe katika vipando lakini akaapa kuwa hatotubeba, kisha akatubeba, akasema Abuu Musa: Basi tukaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamueleza hilo, akasema: “Si mimi niliyekubebeni, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekubebeni Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”
Explanation
Benefits
Inajuzu kutojipa uhakika kwa kusema “Mwenyezi Mungu akipenda” baada ya kiapo, ikiwa kutafanywa kwa nia na kiapo na kukaunganishwa nacho, basi kafara haitohitajika kwa mwenye kuvunja kiapo chake.
Himizo la kuvunja kiapo ikiwa ataona jambo bora kuliko hilo, na atatoa kafara ya kiapo chake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

