Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.
Explanation
Benefits
Nikuwa swala za usiku hazina idadi maalumu; kwa kuwa tamko liliachwa wazi.
Amesema Nawawi: "Swala za usiku na mchana ni rakaa mbili mbili", hadithi hii inachukuliwa kama kubainisha kilicho bora zaidi, nayo ni atoe salamu katika kila rakaa mbili, na sawa sawa ziwe ni sunna za usiku na mchana, na ni sunna atoe salamu kwa kila rakaa mbili.
Amesema Nawawi: Hapa kuna ushahidi kuwa sunna ni kuifanya witiri kuwa swala ya mwisho wa usiku, na kwamba wakati wake unamalizika kwa kuchomoza Alfajiri, na ndio kauli mashuhuri katika madhehebu yetu, na ndivyo lilivyosema jopo la wanachuoni.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

