Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anapoondoka katika swala yake anaomba msamaha mara tatu, na anasema: "Allaahumma antas salaam waminkas salaam, tabaarakta yaa dhal-jalaali wal-ikraam", Anasema Walid: Nikasema kumwambia Auzaiy: Ni vipi unaomba msamaha: Akasema: Unasema: Astagh-firullaah, Astagh-firullaah.
Explanation
Kisha anamtukuza Mola wake Mlezi kwa kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika wewe ni amani, na amani inatoka kwako, umetukuka ewe mwenye utukufu na ukarimu" Mwenyezi Mungu aliyesalimika na kukamilika katika sifa zake, aliyetakasika na kila aibu na mapungufu, na unaomba kutoka kwake Mtukufu amani kutokana na shari za dunia na akhera na si kwa mwingine asiyekuwa yeye, naye Mtukufu kheri zake ni nyingi duniani na akhera, mwenye utukufu na wema na ihisani.
Benefits
Sunna ya kuomba msamaha ili kuziba mapungufu ndani ya ibada na kuipa nguvu ibada na uzembe uliojitokeza ndani yake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

