Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akiomba akisema: "Allaahumma inniy a'udhubika min adhaabil Qabri, wa min adhaabin naari, wamin fitnatil mahyaa wal mamaati, wamin sharri fitnatil masiihiddajjaali" Ewe Mola wangu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na adhabu ya kaburi, na kutokana na adhabu ya moto, na fitina za uhai na za kifo, na kutokana na fitina za masihi dajali".
Explanation
Jambo la kwanza: Kuomba kinga kutokana na adhabu za kaburi.
Jambo la pili: Kuomba kinga ya kuepukana na adhabu ya moto siku ya Kiyama.
La tatu: Kuomba kinga itokanayo na fitina za uhai ikiwemo matamanio ya dunia yaliyoharamishwa na ikiwemo pia shub-ha (utata) wenye kupoteza, na kutokana na fitina za mauti, yaani muda wa kukata roho, tusije kupinda tukatoka katika Uislamu au Sunna, au fitina za kaburini kama maswali ya Malaika wawili.
Jambo la nne:Kuomba kinga zitokanazo na fitina za Masihi Dajali atakeyetokea zama za mwisho, Mwenyezi Mungu atawapa mtihani waja wake kupitia yeye; na Mtume kamtaja kwa jina kutokana na ukubwa wa fitina zake.
Benefits
Kuthibiti uwepo wa adhabu za kaburi nakuwa adhabu hizo ni kweli.
Uhatari wa fitina na umuhimu wa kuomba kinga kwa Mwenyezi Mungu na kuomba dua ya kusalimika nazo.
Kuthibitika kutokea kwa Dajali na ukubwa wa fitina zake.
Sunna ya kusoma dua hii baada ya tashahudi ya mwisho.
Sunna ya kuomba dua baada ya matendo mema.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

