Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".
Explanation
Benefits
Inafaa kuswali katika nguo mbili, moja inasitiri juu ya mwili, na nyingine inasitiri chini yake.
Inapendeza na ni sunna mwenye kuswali awe katika muonekano mzuri.
uwajibu wa kufunika mabega mawili au moja ndani ya swala, akiweza kufanya hivyo, na imesemekana kuwa katazo ni la kujitakasa (mbele ya Mwenyezi Mungu).
Uchache wa yale waliyoyamiliki Maswahaba katika mali, mpaka utakuta mmoja wao hamiliki nguo mbili.
Amesema Imam Nawawi katika maana ya hadithi: Hekima yake nikuwa akijifunga chini na kukawa juu ya mabega yake hakuna kitu basi hatosalimika na kutofunuka uchi wake, tofauti na ambavyo atakaiweka sehemu ya nguo juu ya bega lake, na ni kwa sababu anaweza kuhitaji kuishika kwa mkono wake au mikono yake akashughulishwa na hilo, na ikampita sunna ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua chake, na kuinyanyua kwake pale ambapo ni sheria kuinyanyua, na mengineyo, kwa sababu ndani yake kuna kuacha kusitiri juu ya mwili na sehemu ya pambo, na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukueni pambo lenu katika kila msikiti" [Al-Araf: 31].
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

