القيامة
Al-Qiyamah
The Resurrection
1 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 001
لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti;
2 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 002
وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ
Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika.
3 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 003
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ
Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika?
4 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 004
بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ
Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake.
5 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 005
بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ
Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia?
6 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 006
يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ
Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
7 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 007
فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ
Basi jicho litapo dawaa!
Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka,
8 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 008
وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ
Na mwezi utapo patwa!
Na mwangaza wa mwezi ukapotea,
9 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 009
وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ
Na likakusanywa jua na mwezi!
Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi,
10 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 010
يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ
Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu?
11 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 011
كَلَّا لَا وَزَرَ
La! Hapana pa kukimbilia!
Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe,
12 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 012
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ
Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni.
13 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 013
يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ
Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha.
14 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 014
بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ
Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha.
15 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 015
وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ
Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo.
16 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 016
لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ
Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
Usiuharikishe ulimi wako kwa kuisoma Qur'ani na kujaribu kuihifadhi kwa haraka pale unapo teremshiwa kwa Wahyi.
17 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 017
إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ
Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
Hakika ni juu yetu Sisi kuikusanya hiyo katika kifua chako, na kuithibitisha katika ulimi wako.
18 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 018
فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ
Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
Akikusomea Mjumbe wetu (Jibril) basi nawe ifuatilize kama unavyo isikia.
19 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 019
ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ
Kisha ni juu yetu kuubainisha.
Kisha baada ya hayo ni juu yetu kuibainisha ikiingia tatizo lolote juu yako.
20 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 020
كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ
Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
Wacheni kukanya kufufuliwa, na hilo ni jambo la kweli. Lakini nyinyi mnaipenda dunia na starehe zake,
21 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 021
وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ
Na mnaacha maisha ya Akhera.
Na mnaiacha Akhera na neema zake.
22 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 022
وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ
Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.
23 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 023
إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ
Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.
24 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 024
وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ
Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
Na nyuso nyengine zitakuwapo zimenuna, zimekunjana mno, zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.
25 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 025
تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ
Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
Zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.
26 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 026
كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ
La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
Mna nini na kuipenda dunia ambayo mnaifariki roho inapo fika katika mafupa ya kooni,
27 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 027
وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ
Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
Na walio hudhuria wakasema: Yupo wa kumganga huyu kwa haya aliyo nayo?
28 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 028
وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ
Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
Akayakinisha yule yaliyo mfika mauti kama lililo mshukia ni kuiacha dunia inayo pendwa, na imekwisha mfika shida yake kikomo cha mwisho.
29 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 029
وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ
Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
Na muundi wa mguu umekwisha ambatana na wa pili wakati wa kutoka roho.
30 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 030
إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ
Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
Kwa Mola wako Mlezi tu siku hiyo ndio machungio ya waja, ama Peponi au Motoni.
31 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 031
فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ
Kwa sababu hakusadiki, wala hakuswali.
Binaadamu amekanya kufufuliwa, na kwa hivyo hakumsadiki Mtume wala Qur'ani. Wala hakumtimizia Mwenyezi Mungu faridha za Swala.
32 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 032
وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Bali alikanusha, na akageuka.
Lakini aliikadhibisha Qur'ani, akaipuuza Imani,
33 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 033
ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ
Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
Na akatoka kwenda kwa watu wake wa nyumbani kwa maringo na kujitapa.
34 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 034
أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ
Ole wako, ole wako!
Ewe unaye kadhibisha, utaangamia!
35 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 035
ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ
Kisha Ole wako, ole wako!
Tena utaangamia! Na tena utaangamia, na utaangamia!
36 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 036
أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى
Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
Hivyo anadhani huyu mtu anaye kanya kufufuliwa kuwa ataachwa hivi hivi akiringa tu katika maisha yake, na akisha kufa iwe basi, wala asifufuliwe akahisabiwa kwa vitendo vyake?
37 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 037
أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ
Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
Kwani yeye mtu hakuwa ni tone tu ya manii, ilio jaaliwa kuwemo katika tumbo la uzazi?
38 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 038
ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ
Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
Kisha hiyo tone ikawa kipande cha damu iliyo ganda, na Mwenyezi Mungu akaiumba, akaisawazisha mpaka ikawa na umbo zuri?
39 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 039
فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
Akajaalia namna mbili, mwanamume na mwanamke?
40 - Al-Qiyamah (The Resurrection) - 040