Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
Search and read verified Prophetic hadeeth translations, explanations, benefits, categories and source attribution. Page 3.
Smart instant results tolerate minor spelling mistakes, with every filter in one place.
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hapigwi mtu zaidi ya viboko kumi isipokuwa kama itakuwa katika kutelekeza sheria miongoni mwa sharia za Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, nywele zake zinapigapiga mabega yake, na mabega yake yako mbali mbali, si…
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku…
Kutoka kwa Thabit bin Dhwahaki- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuunga mkono Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chini ya mti, nakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakaye apa juu ya kiapo cha mila isiyokuwa ya uislamu kwa uong…
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yeyote atakaetubebea silaha dhidi yetu, si miongoni mwetu".
Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna…
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo,…
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
Imepokelewa Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Yakrib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapompenda mtu ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda".
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.
Follow any language without creating an account.