Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mimi ndiye mtu niliyekaribu zaidi kwenu nyinyi swala yangu kufanana na swala ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, bila shaka hii ndio ilikuwa swala yake mpaka alipoondoka duniani
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Anasimulia yakuwa yeye alikuwa akitoa takbira katika swala zote za faradhi na zinginezo, ndani ya ramadhani na nje ya ramadhani, anatoa takbira anaposimama, kisha anatoa takbira wakati anarukuu,…

