Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Kuna watu walimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu makuhani, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hawana lolote" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika wao husimulia jambo baadhi ya nyakati na likawa kweli, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Neno hilo huwa limetoka katika ukweli, Jini hulikwapua na kulinong'oneza katika sikio la kipenzi chake mfano wa kuku anavyotetea, hulichanganya na uongo zaidi ya mia moja (100)".
Explanation
Wakasema: Hakika kauli yao huendana na uhalisia katika baadhi ya nyakati, kama ambavyo huelezea kutokea kwa jambo la gahibu ndani ya mwezi fulani siku fulani, na likatokea sambamba na kauli yao.
Akasema -Rehema na amani ziwe juu yake-: Hakika Majini huiba yale wanayoyasikia katika habari za mbinguni, wakashuka kuja kwa watu wao miongoni mwa makuhani wakawaeleza waliyoyasikia, kisha kuhani anaongeza katika yale aliyoyasikia kutoka mbinguni uongo mia moja (100).
Benefits
Mbingu zimehifadhiwa dhidi ya Mashetani kwa kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ili wasije kusikiliza chochote katika wahyi au kinginecho, isipokuwa atakayeiba kusikiliza na akasalimika na kupigwa kimondo.
Majini hujifanyia vipenzi katika binadamu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

