Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
Explanation
Benefits
Kufikisha maji kuna aina mbili: 1- Kufikisha kwa wajibu, nako ni kule ambako udhu hautimii bila kufanya hivyo, na makusudio yake ni kuosha mahala stahiki na kupaeneza. 2- Kufikisha kwa sunna, nako ni kule ambako udhu unaweza kutimia bila kuosha, na makusudio yake ni kile kilichozidi katika wajibu, kama kurudia kuosha mara ya pili na ya tatu, hii ni sunna.
Sunna ya kutawanya vidole vya mikono na miguu miwili wakati wa kuviosha, na kuvitawanya kwake ni kuacha maji yavifikie.
Amesema Twayibi: Bali hapa alijibu Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sunna za udhu; kwa sababu muulizaji alikuwa anajua msingi wa udhu.
Na miongoni mwa mambo yake mazuri Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujali hisia za watu wengine, na kulinda saikolojia zao.
Hadithi ni dalili ya uwajibu wa kusukutua katika udhu.
Hadithi ni dalili ya sunna ya kupita kiasi katika kupandisha maji puani, isipokuwa kwa mfungaji, kwake si sunna; ili kupitiliza huku kusipelekee kuingia maji kooni kupitia puani, yakaharibu swaumu.
Hapa kuna ushahidi kuwa si wajibu kuhama kwa kila aliyesilimu; kwa sababu Banil-Muntafiq na wengineo hawakuhama, bali walituma misafara yao, na hili liko hivyo, ikiwa mtu yuko katika mazingira ambayo anaweza kudhihirisha ndani yake dini.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

