Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Watu wakasema: Sisi tulimsikia, akasema: Huenda nyinyi mnakusudia fitina ya mtu kwa familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndivyo, akasema: Fitina hiyo inafutwa na swala na swaumu na sadaka, lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza fitina ambayo inapiga kama mawimbi ya Bahari? Akasema Hudhaifa: Akawanyamazisha watu wote kwa hilo, nikasema: Mimi, akasema: Nakuapiza kwa Mwenyezi Mungu, umkose baba yako, ni wewe kweli, Hudhaifa, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
Explanation
Benefits
Fitina binafsi ikiwa inahusiana na dini basi hapa mtu kasemwa vibaya; kwa sababu ima iwe ni uzushi au maasi, na ikiwa inafungamana na mambo ya kidunia, basi huu kwake ni mtihani, na la wajibu kwake ni kuwa subira.
Moyo unaathirika kwa fitina zinazopitishwa, na mwenye kuwezeshwa ni yule aliyeongozwa na Mwenyezi Mungu kudumu katika uongofu.
Amesema Nawawi: Amesema Mtunzi wa kitabu Attahriiri: Maana ya hadithi: Nikuwa mtu atakapofuata matamanio yake na akafanya maasi, moyo wake huingia giza kwa kila maasi anayoyafanya, na akiendelea hivyo basi hufitinika na kuondoka nuru ya Uislamu, na moyo kuwa kama mfano wa chungu kikijifunika humwagika kilichomo, na hakiwezi kuingia kitu tena baada ya hapo.
Kauli ya Omari kwa Hudhaifa: (Umkose baba yake) Maana yake: Umedhamiria kweli katika jambo hili, na kaza na ujiandae kujiandaa kwa mtu asiyekuwa na msaidizi.
Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mlango uliofungwa baina ya watu na fitina
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

