HadeethEnc · 1.18.0
Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake
Available translations
Choose an available translation of this Hadeeth
01
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Shuraihi radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini", wakasema: Na ni nani huyo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ambaye hapati amani jirani yake kwa kero zake".
02
Explanation
Aliapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na akasisitiza kiapo chake mara tatu, akasema: Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Wallahi hawezi kuamini, Maswahaba wakamuuliza: Na ni nani ambaye hawezi kuamini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ambaye jirani anahofia usaliti wake na dhulma zake na shari zake.
03
Benefits
Kukanushwa imani kwa yule ambaye jirani yake hapati amani kutokana na dhulma zake na shari zake hili linaonyesha kuwa ni katika madhambi makubwa, na kwamba mfanyaji wake anaupungufu wa imani.
Himizo la msisitizo juu ya kumtendea wema jirani na kuacha kumuudhi kwa kauli au kitendo.
Himizo la msisitizo juu ya kumtendea wema jirani na kuacha kumuudhi kwa kauli au kitendo.
Attribution
[Imepokelewa na Al-Bukhaariy]
Categories
Share
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

