Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake: Kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika misikiti, na watu wawili walipoendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wakakutana kwa ajili yake na wakaachana kwa ajili yake, na mwanaume aliyeitwa na mwanamke mwenye wadhifa na uzuri, akasema: Hakika mimi ninamhofu Allah, na mtu aliyetoa sadaka akaificha mpaka usijue kushoto kwake unachotoa kulia kwake, na mtu aliyemkumbuka Mwenyezi Mungu akiwa faragha, yakabubujika machozi macho yake".
Explanation
Benefits
Amesema bin Hajari katika kauli yake "Katika kivuli chake": Imesemwa kuwa makusudio yake: Ni kivuli cha Arshi yake, na linaonyeshwa hilo na hadithi ya Salmaan iliyoko kwa Saidi bin Mansuri kwa Isnadi hasan "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu chini ya kivuli cha Arshi yake".
Amesema bin Hajari: Na tafsiri nzuri iliyofasiriwa neno muadilifu: Ni yule anayefuata amri za Mwenyezi Mungu kwa kukiweka kila kitu mahali pake, pasina uzembe wala kupita mpaka, na amemtanguliza katika kumtaja kwa sababu ya manufaa yake mapana.
Fadhila za kusubiri swala baada ya swala.
Amesema Nawawi: Hapa kuna himizo la kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kumebainishwa ukubwa wa fadhila zake.
Umetajwa wadhifa na uzuri pekee kwa sababu ya shauku kubwa ya watu katika hayo, na kuyapupia kwao, na ugumu wa kupatikana kwake.
Kilicho bora katika sadaka ni kuficha na kujiweka mbali na kujionyesha, pamoja nakuwa ni sheria kudhihirisha sadaka na zaka, ikiwa zitasalimika na kujionyesha, na zikakusudiwa kuwahimiza wengine katika utoaji na ili mtu mwingine amuige, na kwa ajili ya kudhihirisha nembo ya Uislamu.
Na bila shaka wamepata watu hao neema hiyo kwa sababu ya kutakasa nia zao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwenda kinyume na matamanio ya nafsi.
Kauli yake: "Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu": Kuwadhibiti kwa idadi hii si lengo, bali imepokelewa watu wengine wasiokuwa hawa katika hadithi nyingine miongoni mwa wale atakaowakinga Mwenyezi Mungu chini ya kivuli cha Arshi yake.
Amesema bin Hajari: Kutajwa wanaume pekee katika hadithi hii haina maana yoyote; bali wanawake wanashirikiana nao katika matendo yaliyotajwa, isipokuwa kama itakuwa makusudio ya kiongozi muadilifu ni uongozi mkuu, na kama si hivyo basi kunauwezekano wa mwanamke pia kuingia katika hili pale anapokuwa na familia akawafanyia uadilifu, na anaondolewa katika swala la kudumu msikitini; kwa sababu swala ya mwanamke nyumbani kwake ndiyo bora kuliko kuswalia msikitini, na mbali na hayo basi yaliyobakia yote wanashirikiana na yanapatikana kwao, hata mwanaume aliyeitwa na mwanamke, hili pili linaweza kutokea kwa mwanamke aliyeitwa na mfalme mzuri kwa mfano akakataa kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu pamoja na kuwa anamuhitajia.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

