HadeethEnc · 1.18.0
Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera
Available translations
Choose an available translation of this Hadeeth
01
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera, na atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, Mwenyezi Mungu akamsitiri na akamsamehe, basi Mwenyezi Mungu ni mkarimu zaidi (hawezi) kurudi katika jambo ambalo alikwishalisamehe".
02
Explanation
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."
03
Benefits
Ukubwa wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake na rehema yake.
Kutekeleza adhabu za kisheria katika dunia hufuta dhambi.
Atakayetumbukia katika dhambi ambalo ndani yake ni lazima ajisitiri na kujificha kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na afanye haraka kufanya toba ya kweli.
Kutekeleza adhabu za kisheria katika dunia hufuta dhambi.
Atakayetumbukia katika dhambi ambalo ndani yake ni lazima ajisitiri na kujificha kwa sitara ya Mwenyezi Mungu, na afanye haraka kufanya toba ya kweli.
Attribution
[Imepokelewa na Tirmidhi na bin Majah]
Categories
Share
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

