Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ummu Salama radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema: "Hakuna Muislamu yeyote atakayefikwa na msiba akasema aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu: "Innaa lillaahi wa innaa ilaihi raajiuun" (Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika sisi sote kwake tutarejea) [Baqara: 156], Ewe Mwenyezi Mungu nilipe katika msiba wangu, na unipe badala bora kuliko hili, isipokuwa Mwenyezi Mungu atampa badala bora kuliko hiyo" Akasema: Alipofariki Abuu Salama, nikasema: Ni Muislamu gani atakuwa bora kuliko Abuu Salama? Nyumba ya kwanza aliyohamia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha mimi nikasema maneno hayo, Mwenyezi Mungu akanipa mbadala wake ambaye ni Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Explanation
Benefits
Kuelekeza dua kwa Mwenyezi Mungu katika mambo mazito; kwa sababu kwake ndio kuna mbadala.
Umuhimu wa waumini kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hata isipojulikana hekima yake.
Kheri yote kwa muumini iko katika kutekeleza amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

