Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anapo kufa mwanadamu matendo yake hukatika isipokuwa mambo matatu: Sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema wa kumuombea dua"
Explanation
La kwanza: Sadaka yenye kuendelea thawabu zake na kudumu, isiyokatika, kama wakfu, na kujenga msikiti, na kuchimba visima, na mengineyo.
La pili: Elimu wanayonufaika nayo watu, kama kutunga vitabu vya kielimu, au kama kumfundisha mtu, yule naye akaisambaza elimu hiyo baada ya kifo chake.
La tatu: Mtoto mwema muumini wa kumuombea dua mzazi wake.
Benefits
Yametajwa mambo haya matatu pekee katika hadithi; kwa sababu ndio msingi wa mambo ya kheri, na ndio mambo wanayoyafanya watu wema wengi baada ya kuondoka kwao.
Kila elimu yenye kunufaisha basi hupatikana malipo kwa elimu hiyo, lakini kilele chake ni elimu ya kisheria na elimu za msingi kwake.
Elimu ndiyo yenye manufaa zaidi kati ya haya matatu; Kwa sababu elimu inamnufaisha mtu anayeisoma, elimu inahusisha kuihifadhi Sheria, inawanufaisha watu kwa ujumla, na ni pana zaidi na ni ya jumla, kwa sababu anajifunza kutoka katika elimu yako aliyepo wakati wa uhai wako na atakayekuwepo baada ya kufa kwako.
Himizo la kulea watoto wema; Wao ndio wanaowanufaisha wazazi wao Akhera, na miongoni mwa manufaa yao ni kuwaombea dua.
Himizo la kuwatendea wema wazazi wawili baada ya kufa kwako, nao ni katika wema ambao mtoto anafaidika nao.
Dua inamnufaisha maiti hata kama haikutoka kwa mtoto, lakini katajwa mtoto pekee kwa sababu ndiye atakayeendelea kumuombea dua mtu mara nyingi mpaka kufa kwake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

