Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Watamkisheni maiti wenu (neno) Laa ilaaha illa llaah".
Explanation
Benefits
Inachukiza kukariri sana kumtamkisha aliyefikwa na umauti, na kumlazimisha endapo atalitamka, au ikafahamika kuwa ametamka; ili wasimsumbue akatamka maneno yasiyofaa.
Amesema Nawawi: Na akilitamka mara moja basi asilikariri tena isipokuwa kama atatamka baada yake maneno mengine, hapo litarudiwa tena ili liwe neno lake la mwisho.
Hadithi inakusanya kuhudhuria mbele ya aliyefikwa na umauti ili kumkumbusha na kumliwaza na kumfunga macho na kusimamia haki zake.
Si sheria kumtamkisha mtu baada ya kifo na kaburini baada ya mazishi; kwa sababu ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutolifanya hilo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

