Atakayeswali swala yetu na akaelekea kibla chetu na akala kichinjwa chetu basi huyo ni Muislamu mwenye dhima ya Mwenyezi Mungu na dhima ya Mtume wake, msimfanyie hiana Mwenyezi Mungu katika dhima yake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayeswali swala yetu na akaelekea kibla chetu na akala kichinjwa chetu basi huyo ni Muislamu mwenye dhima ya Mwenyezi Mungu na dhima ya Mtume wake, msimfanyie hiana Mwenyezi Mungu katika dhima yake".
Explanation
Benefits
Mambo ya watu huchukuliwa kwa dhahiri pasina undani, atakayedhihirisha nembo za dini basi zitatekelezwa kwake hukumu za Waislamu madamu hajadhihirisha kinyume na hivyo.
Amesema bin Rajab: Ametaja kuelekea kibla kama ishara yakuwa ni lazima kuitekeleza swala ya Waislamu iliyowekwa kisheria ndani ya kitabu chao kilichoteremshwa kwa Nabii wao, nayo ni swala ya kuelekea kibla, na vinginevyo atakayeswali kwa kuelekea Palestina baada ya kufutwa kwake kama Mayahudi au Mashariki kama Wakristo, huyo si Muislamu, hata kama atashuhudia kwa shahada ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu.
Hapa kuna dalili ya utukufu wa kuelekea kibla katika swala, kwa sababu hakutaja katika sharti za swala sharti nyingine, kama twahara na nyinginezo.
Amesema bin Rajab: Kutaja kula kichinjwa cha Waislamu kuna ishara kuwa ni lazima kushikamana na sheria zote za Uislamu za wazi, na miongoni mwa kubwa zake ni kula kichinjwa cha Waislamu, na kukubaliana nao katika kichinjwa chao, atakayekataa kula huyo si Muislamu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

