Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika, (Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: Allaahumma'swimnii minash-shaitwaanir-rajiim", (Ewe Mwenyezi Mungu nikinge dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Na katika riwaya ya Al-Haakim: "Na akitoka amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu nilinde dhidi ya Shetani aliyelaaniwa".
Explanation
Benefits
Dua hii ni kwa misikiti yote, hata Msikiti mtukufu wa Makka.
Rehema zimetajwa maalumu wakati wa kuingia, na kukingwa na Shetani wakati wa kutoka: Ni kwakuwa mwenye kuingia anashughulika na kile kinachomuweka karibu na Mwenyezi Mungu na karibu na Pepo yake ikawa ni mahala pazuri pa kutaja rehema, na akitoka anakwenda katika dunia na yote yaliyomo miongoni mwa mapumbao na vyenye kushughulisha, ikawa ni sehemu nzuri ya kuomba ulinzi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kuhifadhiwa kutokana na Shetani.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

