Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.
Explanation
Benefits
Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa tabia njema na upole, kiasi kwamba alikuwa akikaa na Maswahaba zake, na akisikiliza mazungumzo yao na simulizi zao, na anatabasamu kwa sababu yake.
Inafaa kufanya mazungumzo na kukumbushia enzi za ujinga msikitini.
Inafaa kucheka na kutabasamu; kwa sababu kilichokatazwa ni kukithirisha kucheka.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

