Funguo za mambo ya ghaibu ni tano
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Funguo za mambo ya ghaibu ni tano, "Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua. Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari".
Explanation
Benefits
Amesema Assindi: Kauli yake: "Funguo za mambo ya ghaibu ni tano", Yameitwa mambo haya matano: Funguo za ghaibu; kwa sababu mwenye kuwa na mambo haya matano basi anamiliki ghaibu yote, yakawa ni sawa na mambo yanayofunguliwa kwayo hazina za ghaibu.
Amesema bin Hajari Abuu Hamza: Ameeleza kwa neno funguo ili kusogeza karibu jambo hili kwa msikilizaji; kwa sababu kila kitu kilichowekwa pazia baina yake na wewe basi kitakuwa kimefichika kwako, na kuweza kufikia kukijua kwa kawaida ni kupitia mlangoni, mlango ukifungwa itahitajika funguo, ikiwa kitu ambacho mtu hawezi kuona ghaibu isipokuwa kupitia hicho hajui mahali kilipo, ataweza vipi kujua ghaibu.
Amesema bin Abii Hamza: Sababu na hekima ya kuyafanya kuwa ni mambo matano ni ishara ya kuwakusanya walimwengu ndani ya hayo.
Inawezekana Mwenyezi Mungu kuwaonyesha ghaibu baadhi ya Mitume, kwa hekima toka kwake Mtukufu
Ubatili wa tabiri za waaguzi na makuhani katika kujipa kwao kujua elimu ya ghaibu, na kwamba mwenye kudai kujua elimu ya mambo aliyojipwekesha nayo Mwenyezi Mungu kwa kuyajua, basi atakuwa amefanya muongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na Qur'ani tukufu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

