bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Ilipoteremka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ni wa Mwenyezi Mungu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Mwenyezi Mungu anakijua, na atawahesabu nacho. Atamsamehe anayemtaka na atampatiliza anayemtaka. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu" [Al-Baqara: 284], anasema: Likawa gumu sana hilo kwa Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu tumepewa jukumu la matendo tunayoyaweza, kama Swala, Swaumu, na Jihadi, na Sadaka, na imeteremka juu yako aya hii wala hatuiwezi, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Je hivi mnataka kusema kama walivyosema watu wa vitabu viwili kabla yenu, tumesikia na tumeasi? bali semeni: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako", wakasema: Tumesikia na tumetii tunataraji msamaha toka kwako ewe Mola wetu Mlezi, na marejeo ni kwako, walipoisoma kauli hiyo, zikadhalilika ndimi zao, akateremsha Mwenyezi Mungu punde tu baada ya hapo: "Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, (pia wameamini hivyo) wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na husema tumesikia na tumetii, tunakuomba msamaha Mola wetu na marejeo ni kwako" [Baqara: 285] walipofanya hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu akaifuta, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mwenyezi Mungu hailazimishi nafsi yoyote isipokuwa yaliyo sawa na uweza wake. (Faida ya) yale iliyochuma (nafsi hiyo) ni yake na hasara ya yale iliyochuma ni juu yake. (Husema); Mola wetu usitutese kama tukisahau au tukikosa" [Al-Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "Mola wetu na usitubebeshe mzigo kama uliowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" Akasema: Ndiyo "Mola wetu usitutwike tusiyoyaweza" [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo "na utusamehe na utufutie na uturehemu, Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tusaidie juu ya watu makafiri." [Baqara: 286] Akasema: Ndiyo.
Explanation
Benefits
Kuthibitika kufutwa kwa aya ndani ya Qur'ani tukufu, na kwamba ndani ya Qur'ani ziko aya zinazosomwa lakini hukumu yake ilifutwa haifanyiwi kazi.
Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na utiifu wao na kujisalimisha kwao katika amri za Mwenyezi Mungu, na kutekeleza kwao amri ya Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa na hofu kubwa juu ya Umma wake usijekupita njia za Umma zilizotangulia kwa kuyakataa yale waliyopewa miongoni mwa amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Uwajibu wa kujisalimisha katika amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na tahadhari ya kuleta upinzani katika amri zake, na kwamba kitendo hiki kuna kujifananisha na watu wa kitabu.
Kumebainishwa ubora wa Umma huu juu ya Umma zilizotangulia, kiasi ambacho wao walisema kuwaambia Manabii wao: Tumesikia na tumeasi, na Umma huu ulisema: Tumesikia na tumetii.
Ubora wa Umma katika kuondolewa uzito juu yake na kujibiwa kwa dua ya kutoadhibiwa kwa kusahau au kukosea, na kuondolea ugumu juu yake uliokuwa kwa wale waliokuwa kabla yao, na kutobebeshwa kwake yale usiyoyaweza.
Mwenyezi Mungu Mtukufu hatubebeshi tusiyoyaweza, na wala hatulazimishi ila kwa kadiri ya uwezo wetu, na kwamba wasi wasi wote unaozunguka ndani ya vifua ikiwa hatutouendekeza, na hatukutulizana kwake, na hatukuufanyia kazi, basi huo haudhuru.
Dua hii ametueleza Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na waumini, na akaiweka ndani ya kitabu chake; ili iwe ni dua kwa wale watakaokuja baada ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, basi ni katika dua ambazo inapaswa kuzihifadhi, na kuziomba kwa wingi.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

