“Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kuwa mwanamume mmoja alimsikia mtu akisoma: "Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee." Huku akiirudiarudia. Ilipofika asubuhi, alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake, na akamueleza hilo. Na ni kana kwamba mwanamume huyo aliona jambo hilo ni jambo dogo. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika, hiyo ni sawa na theluthi moja ya Qur'ani."
Explanation
Benefits
Inafaa kusoma katika kisimamo cha usiku walau kwa aya chache na kuzirudia rudia, na kutokuziona ndogo.
Amesema Al-Maaziri: Inasemekana maana yake: Nikuwa Qur'ani iko katika sehemu tatu; visa na hukumu na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu, na (Qul-huwallaahu Ahad) imejikita kwa ajili ya sifa za Mwenyezi Mungu, hivyo ni theluhti, na ni moja kati ya sehemu tatu, na imesemekana maana yake kuwa: Thawabu za kuisoma kwake hulipwa mara dufu kwa kiasi cha kusoma theluthi ya Qur'ani bila kuzidishwa.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

