Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Hazim bin Dinari: Anasimulia kuwa watu fulani walikuja kwa Sahli bin Sa'di As-saaidi, wakiwa wamepatwa na shaka kuhusu mimbari (ya Mtume) ilitengenezwa kwa mti gani, wakamuuliza kuhusu hilo, akasema: Wallahi mimi ninajua imetokana na mti gani, na niliiona tangu siku ya kwanza ilipowekwa, na siku ya kwanza kuikalia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, aliagiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa fulani -Mwanamke aliyekuwa mke wa mmoja kati ya Maanswari (Watu wa Madina) -Sahli alimtaja kwa jina lake-: "Muamrishe kijana wako seremala anitengenezee kibao niwe nakalia ninapo zungumza na watu", akamuamrisha akatengeneza kutokana na mti wa Twarfa (Mti mfano wa mkaratusi) hupatikani msituni, kisha akaileta, yule mama akaiagiza kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akaamrisha ikawekwa hapa, kisha nikamuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa juu yake na akatoa takbira (Allahu Akbaru) akiwa juu yake, kisha akarukuu akiwa ju yake, kisha akashuka kinyumenyume akasujudu mwishoni mwa mimbari, kisha akarudi, alipomaliza swala yake akawageukia watu kisha akasema: "Enyi watu! Bila shaka nimefanya hivi ili muige na mjifunze swala yangu".
Explanation
Benefits
Kufaa kusali juu ya Mimbari kwa ajili ya kufundisha, na inafaa kwa imamu kuwa juu kuliko maamuma kukiwa na haja.
Inafaa kuwaomba msaada watu wenye ufundi fulani katika haja za waislamu.
Inafaa kufanya harakati ndogo ndani ya swala kukiwa na haja.
Inafaa maamuma kumtazama imamu wake akiwa ndani ya swala; ili ajifunze kutoka kwake, nakuwa hilo haliondoi utulivu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

