Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama wingi wa nyota mbinguni na sayari zake
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abii Dharri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hicho chombo cha Birika kiko vipi? Akasema: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, kwa hakika vyombo vyake ni vingi kama wingi wa nyota mbinguni na sayari zake eleweni vyema kuwa kung'aa kwake kutakuwa katika usiku usio na mwezi, pako safi, vyombo vya peponi atakaye kunywa katika vyombo hivyo hatopatwa na kiu milele wala kiu hakitomrudia, na maji hayo yanaruka na kububujika kupitia mabomba mawili yaliyo juu ya peponi, yeyote atakaye kunywa katika Birika hilo hatopatwa na kiu, upana wake ni sawa na urefu wake ambao ni sawa kutoka Amman mpaka Aila (Ni katika miji ya Jordan, baina yake ni km 330) maji yake ni meupe mno kuliko maziwa, na ni matamu kuliko asali."
Explanation
Benefits
Ukubwa wa Birika na urefu wake na upana wake na wingi wa vyombo vyake.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

