Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.
Explanation
Atakayesema wakati wa jioni halitomfika balaa la ghafla mpaka afike asubuhi, na atakayesema wakati wa asubuhi balaa halitomfika la ghafla mpaka afike jioni.
Akaipatia riwaya ya hadithi ya Abana bin Othman Al-Falij; Nayo ni kudhoofika kwa baadhi ya upande wa mwili, yule bwana aliyesikia kwake hadithi akamtazama Abana kwa kustaajabu?! Abana akasema kumwambia yule bwana: Mbona wanitazama?! Wallah sijamzulia uongo Othman, wala Othman hajamzulia uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini leo yamenifika yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwangu kuyasema, nimepatwa na hasira nikasahau kusema maneno haya yaliyotajwa.
Benefits
Nguvu kubwa ya yakini kwa wema wa mwanzo kwa Mwenyezi Mungu na kuyasadikisha kwao yale aliyoyaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Miongoni mwa faida za kufanywa dhikri ziwe za asubuhi na ajioni ni kuondoa hali ya kughafilika kwa muislamu na kuvuta kwake picha endelevu kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Kwa kadiri inavyokuwa imani ya mtajaji Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wake na kuhudhurisha kwake moyo, pamoja na kutakasa nia na yakini ndivyo itakavyozidi kupatikana athari ya dhikri.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

