Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwapige vijakazi wa Mwenyezi Mungu" Akaja Omari kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hivi sasa wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, basi akaruhusu kuwapiga, baada ya muda wakaanza kuzunguka katika familia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika wamekuja katika familia za Muhammad wanawake wengi wakiwashitakia waume zao, (wanaume) hao si bora kati yenu".
Explanation
Benefits
Alifanya Mwenyezi Mungu Mtukufu kipigo kuwa hatua ya mwisho katika suluhisho la ujeuri, akasema: "Na wale mnaochelea kutoka kwao katika utiifu, waaidhini (wanasihini), na wahameni katika malazi, na wapigeni. Basi wakiwatii, msitafute njia yoyote dhidi yao. Hakika, Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa" [An-Nisaai: 34], na njia hizi tatu zimepangwa kwa utaratibu, na si zote kwa wakati mmoja, ataanza kwa nasaha na mawaidha, na kumkubusha, ikiwa itazaa matunda basi Alhamdulillaah, na isipoleta tija amuhame kitandani,, isipoleta tija, ampige kipigo cha kuadabisha nasi cha kulipa kisasi.
Mwanaume ni msimamizi katika nyumba yake, anawajibu wa kuwalea na kuwaadabisha kwa hekima na mawaidha mazuri.
Inafaa msomi kujirudi katika majibu yake; pale anapojua matokeo yake na mwisho wake.
Inafaa kuweka kikao cha majadiliano na kiongozi au mwanachuoni, endapo alipatwa madhara anayeshitaki.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

