Kamlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa, na mwenye kuchora chata na mwenye kuchorwa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Kamlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa, na mwenye kuchora chata na mwenye kuchorwa.
Explanation
Benefits
Katazo la kusaidizana katika madhambi.
katazo la kubadili umbile la Mwenyezi Mungu; kwa sababu kufanya hivyo ni udanganyifu na ni ghushi.
Kufaa kumlaani aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa mfumo wa ujumla.
Inaingia katika kuunga nywele katika zama zetu hizi kuvaa mawigi, nalo ni jambo la haramu, kwakuwa kuna kujifananisha na makafiri na udanganyifu na ghushi na uongo.
Amesema Khattwabi: Hakika imekuja ahadi ya adhabu kali katika mambo haya; kwakuwa ndani yake kuna ghushi na udanganyifu, na lau lingeruhusiwa lolote katika haya ingelikuwa njia ya kuhalalisha mengine katika aina za ghushi, na kwakuwa ndani yake kuna kubadili maumbile, na katika hilo kuna ishara ya hadithi ya bin Masudi kwa kauli yake: "Wenye kubadili maumbile ya Mwenyezi Mungu", na Allah ndiye mjuzi zaidi.
Amesema Nawawi: Nalo ni jambo la haramu kwa mfanyaji na mwenye kufanyiwa, na sehemu aliyochorwa inakuwa najisi, ikiwa ataweza kuiondoa kwa tiba basi ni wajibu kwake kufanya hivyo na isipowezekana basi aiondoa kwa upasuaji, ikiwa atahofia kuharibika au kukosa kiungo au matumizi yake au chochote kibaya katika kiungo kinachoonekana basi haitokuwa wajibu kwake kuiondoa, na akitubia hatobaki na madhambi, na asipohofia chochote katika hayo basi ni lazima kwake, na atakuwa ameasi akichelewesha kuiondoa. Mwisho.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

