Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Explanation
Benefits
Ahadi kali kwa anayechukua mali za watu kwa dhulma.
Hakuna atakayedhulumu isipokuwa atakuja na kila alichodhulumu siku ya Kiyama.
La wajibu kwa muajiriwa katika kazi yoyote miongoni mwa kazi za nchi atimize majukumu aliyopewa, na hatakiwi kuchukua zawadi katika kile kinachohusiana na kazi yake, na akichukua basi akiweke katika benki ya Waislamu, na haifai kuichukua kwa matumizi yake binafsi, kwa sababu hilo ni njia ya kwenda katika shari na kupoteza amana.
Amesema bin Battwal: Hadithi imeonyesha kuwa zawadi kwa mfanya kazi inakuwa ni shukurani kwa wema wake, au kwa ajili ya kujipendekeza kwake, au kumtaka asitende haki, akaashiria Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa anachozawadiwa yeye katika hivyo yuko sawa na Waislamu wengine, hana ubora kuliko wao katika hicho, na kwamba haifai kujipendelea.
Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Kumebainishwa kuwa zawadi zote za wafanya kazi ni haramu na ni wizi; kwa sababu atakuwa kafanya hiana katika uongozi wake na amana yake, na ndio maana akataja katika hadithi katika adhabu yake na kumbebesha kwake kile alichozawadiwa siku ya Kiyama, kama alivyotaja mfano kwa mwenye kuficha mali, na amebainisha rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii sababu ya kuharamisha zawadi, ambayo ni uongozi, kinyume na zawadi ya mtu ambaye si mfanya kazi, kwani hiyo inafaa kuchukua.
Amesema bin Munir: Inachukuliwa katika kauli yake: "kwa nini asingekaa nyumbani kwa baba yake na mama yake" Kuwa inafaa kupokea zawadi kutoka kwa yule aliyekuwa akimpa zawadi kabla ya hapo, amesema bin Hajar: Na haifichikani kuwa mahali pake nikuwa isizidi kiwango cha kawaida.
Mfumo wa Mtume katika utoaji wa nasaha, ni kuzungumza kwa watu wote, na si kumtangaza mtu.
Amesema bin Hajari: Hapa inaonyesha kuwa ni sheria kumkagua aliyepewa dhamana.
Amesema bin Hajari: Na inaonyesha kuwa inafaa kumkemea aliyekosea.
Inapendeza kunyanyua mikono katika dua.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

