Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe".
Explanation
Benefits
Fadhila za vikao ambavyo anatajwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, na kumtaja Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, nakwamba vikao ambavyo havina hayo ni vikao vibaya kwa watu siku ya Kiyama.
Tahadhari iliyotajwa ya kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu haishii katika vikao pekee, bali inaenea katika sehemu zingine, amesema Nawawi: Ni machukizo kwa atakayekaa mahali aondoke bila kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake.
Masikitiko yatakayotokea siku ya Kiyama: Ima ni kwa sababu ya kupoteza malipo na thawabu kwa kutofaidika na wakati kwa kumtii Mwenyezi Mungu, na ima ni kwa madhambi na adhabu kwa kuutumia wakati kwa kumuasi Mwenyezi Mungu.
Tahadhari hii ni pale kughafilika kutakapokuwa ni kwa mambo ya halali, je, ni vipi vikiwa vikao vya haramu ambavyo ndani yake kuna utesi na usengenyaji na mengineyo?!.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

