Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri,
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri, Pupia yenye manufaa na wewe, na utake msaada kwa Allah na wala usishindwe, na likikusibu jambo usiseme: Lau ningelifanya kadha basi ingelikuwa kadhaa wa kadhaa, lakini sema: Hili ni kwa makadirio ya Allah naye hufanya alitakalo, maana neno "Lau" hufungua matendo ya shetani".
Explanation
Benefits
Inapendeza kuwa na nguvu katika matendo; kwani hupatikana faida kwa matendo hayo ambayo haipatikani kukiwa na udhaifu.
Mwanadamu anatakiwa apupie katika yale yenye kumnufaisha, na aache yasiyomnufaisha.
Ni wajibu kwa muumini atake msaada wa Mwenyezi Mungu kwake katika mambo yake yote, na wala asiitegemee nafsi yake.
Kuthibiti uwepo wa mipango na maamuzi ya Mwenyezi Mungu (kadhaa na kadari), nakuwa hilo halipingani na swala la mtu kufanya sababu na kwenda kutafuta mambo mazuri na ya kheri.
Katazo la kusema: "Lau" kwa njia ya kulalamika wakati wa kupatwa na mitihani, na uharamu wa kupingana na maamuzi na mipango ya Allah Mtukufu.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

