Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: "Alikuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- zinapoingia siku kumi (za mwisho wa ramadhani) anauhuisha usiku, na anawaamsha watu wake, na anaongeza juhudi na anakaza kikoi".
Explanation
Benefits
Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Nikuwa inapendeza kuzidisha katika ibada mbali mbali katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, na kupendeza kuhuisha siku zake kwa ibada mbali mbali.
Yampasa kila mja awe na pupa kwa familia yake ya kuwaamrisha kufanya ibada, na awe mvumilivu juu yao.
Kufanya mambo ya heri kunahitaji uthubutu na subira na kuvumilia.
Amesema Nawawi: Wametofautiana wanachuoni katika maana ya (Kukaza kikoi) wakasema: Ni kuongeza juhudi katika ibada zaidi ya kawaida yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati zingine, na maana yake: Ni kujipinda katika ibada, husemwa: Jambo hili nimelifungia kikoi, yaani: Nimelidhamiria na nimetenga muda wangu kwa ajili yake, na wamesema wengine: Ni fumbo la kujitenga na wanawake kwa ajili ya kushughulika na ibada.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

