Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imepokewa kutoka kwa Omar Bin Khattwab- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia, atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, (basi malipo yake yatakuwa) ni kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na atakayekuwa kuhama kwake ni kwa ajili ya kuipata dunia, au kwa ajili ya mwanamke atakaemuoa, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kile alichokiendea." Na lafudhi ya Bukhari: "Hakika matendo yote huzingatiwa nia, na hakika kila mtu hulipwa kwa lile alilonuia."
Explanation
Kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akapiga mfano wa kuweka wazi namna gani nia inaathiri matendo pamoja nakuwa huonekana yote yako sawa katika muonekano wa juu, akaweka wazi kuwa atakayekusudia katika kuhama kwake na kuacha nchi yake ni kutafuta radhi za Mola wake, basi kuhama kwake kutakuwa ni kwa kisheria na kunakubalika, atalipwa kwa sababu ya ukweli wa nia yake, na atakayekusudia kwa kuhama kwake ni kupata masilahi ya kidunia, kama mali, au cheo, au mke, basi hatopata kwa kuhama kwake huko zaidi ya manufaa aliyoyakusudia, na wala hatokuwa na fungu la malipo na thawabu.
Benefits
Matendo ambayo hutumika kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwayo, akiyafanya muislamu mtu mzima kwa njia ya mazoea hawezi kuwa na thawabu juu yake, mpaka akusudie kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo hayo.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

