Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote".
Explanation
Benefits
Mwenyezi Mungu amewatengea wafungaji mlango katika milango minane ya Pepo, watakapouingia utafungwa.
Kumebainishwa kuwa Pepo inamilango.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Wako wapi wafungaji", yaani: Wenye kukithirisha kufunga, kama mtu muadilifu na dhalimu, husemwa kwa mtu aliyezoea hilo, na si kwa mwenye kufanya hilo mara moja.
"Rayyan" Yaani: Mwenye kukata kiu; kwa sababu wafungaji hupata kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi zenye joto la muda mrefu; watalipwa kwa kuitwa mlango huu kwa kile kilichokuwa kinawahusu wao, mlango wa Rayyan, na imesemekana kuwa Rayyan ni wingi wa kulowesha koo kinyume cha kiu, na umeitwa hivyo; kwa sababu ndio malipo ya wafungaji kwa kiu yao na njaa yao.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

