Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Ma'adan Bin Abi Twalha Alya'mary amesema: Nilikutana na Thauban muachwa huru wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake nikasema: 'Niambie matendo nitakayo yafanya (iwe sababu kwa Allah) kuniingiza Peponi' au alisema, nikasema: matendo mazuri yanayopendeka zaidi kwa Allah, akanyamaza, kisha nikamuuliza akanyamaza, kisha nikamuuliza kwa mara ya tatu akasema: Nilimuuliza hayo Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Shikamana na kusujudu kwa wingi kwa ajili ya Allah, kwani hakika wewe huta sujudu kwa ajili ya Allah isipokuwa Allah atakupandisha kwa sijida hiyo daraja, na atakufutia kwa sijida hiyo makosa" Akasema Maadan: Kisha nikakutana na Abuudardaa nikamuuliza, akanambia mfano wa hayo alionambia Thauban.
Explanation
Basi rehema na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia muulizaji: Dumu na sijida kwa wingi, kwani kila unapomsujudia Mwenyezi Mungu anakunyanyua daraja kwayo, na anakusamehe dhambi kwa sababu ya sijida hiyo.
Benefits
Kumebainishwa uelewa wa Maswahaba na elimu yao kuwa pepo haipatikani -baada ya huruma ya Mwenyezi Mungu- isipokuwa kwa matendo.
Kusujudu ndani ya swala ni katika sababu kubwa za kunyanyuliwa daraja, na kusamehewa madhambi.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

