Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi
Choose an available translation of this Hadeeth
Hadeeth text
Kutoka kwa Imran bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".
Explanation
Benefits
Malipo kuongezeka kwa kuzidi matamshi ya salamu.
Ukamilifu katika kutoa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na namna nzuri katika kujibu: Ni "Waalaikumus salaam warahmatullaahi wabarakaatuh".
Daraja za kutoa salamu na kujibu zinatofautiana, vile vile malipo yanatofautiana.
Kuwafundisha watu kheri na kuwatanabahisha ili kufanya lililobora zaidi.
Amesema bin Hajari: Ikiwa atazidisha mwenye kuanza "Warahmatullah" basi ni sunna kwake "wabarakaatuh", na ikiwa atazidisha "wabarakaatuh" je ni sheria pia kuzidisha wakati wa kujibu? Na vile vile ikiwa atazidisha mwenye kuanza "wabarakaatuh" je ni sheria kwake kufanya hivyo, ameitoa Maliki katika Muwattwa'a kutoka kwa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Salamu imeishia katika baraka.
Attribution
Categories
Share hadeeth
Sharing options · 0 Total shares

